Daraja linalogharimu nusu billioni kukamilika mwishoni mwa mwaka huu

Serikali imeahidi kurejelea ujenzi wa daraja la Enziu ili kukamilisha mradi huo. Imesema tayari imeweka mpango na mikakati kabambe ya kuendelea kumaliza kujenga daraja katika mto Enziu ambalo linatarajiwa kugharimu serikali zaidi ya shillingi nusu billioni.

Akizungumza jana na wanahabari, mbunge wa Mwingi ya Kati Bw. Gideon Mulyungi alidokeza kwamba mazungumzo tayari yamefanyika kati ya serikali na mwanakandarasi aliyepewa kandarasi hiyo na inatarajiwa ujenzi wa daraja kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

“Mazungumzo yamekamilika ,mwanakandarasi ameanza kazi na anatarajiwa kumaliza ujenzi mwisho wa mwaka huu, serikali itamsaidia kumaliza kazi kwa wakati, ,alisema Mulyungi.

Miezi miwili liyopita, Afisa Mkuu Mshirikishi eneo la Mashariki Evans Achoki alitoa onyo na kutaka mwanakandarasi amalize ujenzi wa mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kuipa sura mpya na kupunguza ajali katika mto huo.

“Tunataka mwanakandarasi amalize mradi huu kabla ya mwisho wa mwaka huu,kwani tunatumaini itasaidia kupunguza ajali nyingi ambazo zimeshuhudiwa katika eneo hili,”alisema Achoki.

Aliongeza kwamba muda wa miezi kumi aliyopewa mwanakandarasi kumaliza mradi huo unazidi kuyoyoma na ni sharti atie bidii kumaliza ujenzi kwa wakati ufao

Hii ni matumaini kubwa kwa wenyeji wa kaunti ya Kitui kwani Mto wa Enziu ulikatiza maisha ya wengi na daraja hilo litasaidia kuzuia maafa zaidi.

Mwaka jana, Basi lilokuwa likibeba waumini wa Kanisa katoliki ya Mwingi liliwezwa na mikondo ya maji yenye nguvu, likapinduka na kuzama ndani ya mto huo wa Enziu na kusambambisha vifo vya watu 32 .

admin

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *