Tume ya Amani na Maridhiano yaanzisha Kampeni za amani Kilifi

Tume ya Amani na Maridhiano inchini (NCIC) imeanzisha rasmi kampeni za kuhamasisha umma kudumisha amani wakati huu taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Kampeni hizo zikiongozwa na Kamishna wa tume hio, bwana Philip Okundi, zimefanyiwa uzinduzi mjini Kilifi, wakilenga kutembea vitongoji vyote, ili kuwarai wananchi kuepuka kuzua vurugu baada ya matokea ya uchaguzi kutangazwa.

Kauli mbiu ya kampeni hio ikiwa ni ‘uchaguzi bila noma’ inalenga kusisitiza umuhimu kupiga kura bila chuki na uhasama miongoni mwa jamii humu inchini.

“Wakati huu tunaenda kwa uchaguzi mkuu, na uchaguzi ni kitu muhimu zaidi kwa nchi yote. Ndio mahali nchi yote iko tayari kwa mabadiliko ambayo itashughulika na maisha ya watu. Wakati huo lazima sisi wanakenya wote tufikirie zaidi nia ya kutafuta yule ambae ataleta amani,” alisema bwana Okundi.

Akizungumza na wanahabari baada ya uzinduzi huo, bwana Okundi alidokeza kwamba mbali na kuhamasisha wananchi kuzingatia amani, tume hio imeweka mikakati kabambe, ya kufuatilia na kudhibiti semi zinazoweza kuleta mhemko na kuzua vurugu.

“Tumewaajiri watu kila mahali, na wako na mitambo fulani ambayo itagundua nani anayaeneza hii mambo ya semi za chuki, mambo inayoleta vurugu, nani anazungumza wapi na kila kitu kitajulikana,” alisema.

Aidha alifichua kwamba tume hio iko na chumba maalum cha kusoma, kusikikiza na kuchunguza semi zote zinazotishia amani kutoka pande zote nchini, ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Kampeni hizo zimehusisha washikadau mbali mbali ikiwemo wizara za serikali, makanisa, tume ya uchaguzi IEBC, tume ya usajili wa vyama, kamati za kiusalama, ili kuhakikisha ufanisi mkubwa wa shughli hio.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na Amani, hasa wakati huu wa uchaguzi ndiposa tunaleta washirika wote katika mikakati ya kuhakikisha tunaeneza hii agenda ya amani,” alisema Jeremiah Were, mkurugenzi wa Kamati ya uongozi wa Taifa, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya amani Kilifi.

Wananchi walioshuhudia kuanzishwa kwa msafara wa kutangaza amani nje ya, Chuo Kikuu Cha Pwani, mjini Kilifi, walielezea furaha yao kuona juhudi za serikali kuleta amani na kuhimizana wenyewe kudumisha amani katika kaunti hio.

Kampeni za amani sawia na hizo zimefanyika katika kaunti zingine ikiwemo Mombasa, Nairobi, Nakuru, Kericho na Kisumu, katika juhudi za kuhakikisha sehemu zote nchini zinabaki na utulivu.

admin

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *