Wakaazi wahimizwa kudumisha amani

Viongozi wa siasa wanaowania nyadhfa mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa Agosti wamewataka wakaazi wazingatie umuhimu wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa Gavana Lee Kinyanjui ambaye anaomba kupewa zamu yake ya pili na wa mwisho katika nyadhfa hii kupitia chama cha Jubilee, amani ni kiungo muhimu katika maendeleo na hivyo basi wale wanaopagnia kuitatiza watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kinyanjui aliendelea kusema kuwa serikali ya kaunti itaimarisha upigaji doria katika maeneo mengi kwa minajili ya kupunguza hali tete zinazoshuhudiwa wakati na baada ya uchaguzi.

Aliwanyoshea kidole wanasiasa walio na nia potovu ya kuwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila akisema kuwa viongozi wa sampuli hii hawafai kupewa fursa ya kuongoza kamwe.

Hata hivyo, aliwashauri kutokana na kuwepo kwa ushawishi wao mkubwa kwa wananchi, wanapaswa kutumia nafasi hio kuunganisha wakaazi mara kwa mara.

Mratibu wa chama cha Jubilee eneo la Kuresoi Njuguna Gichamu alisisitiza umuhimu wa kuilinda amani wakati wote akiwaomba wanasiasa kufanya kampeini zao kwa utulivu.

Aliendelea kusema kuwa hali ya ghasia kuzuka mara kwa mara baada ya uchaguzi ni hali inayofaa katazwa kabisa na wakaazi kuwa mstari wa mbele katika kueneza upendo katika jamii.

Wanasiasa hawa walikuwa wakiongea katika hafla ya mazishi ya mhubiri mmoja wa kanisa eneo la Murinduko, wadi ya Nyota, mzee Stephen Muhoho.

Muhoho alihubiri amani ya hivyo basi watamuenzi kwa kuhakikisha kuwa amani inadumu wakati wote.

admin

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *