Bunge la kaunti ya Elgeyo Marakwet lavunjwa

Bunge la kaunti ya Elgeyo Marakwet lilipitisha miswada 15 tangu lilipoanza shughuli zake mnamo mwaka wa 2017.

Kati ya miswada hiyo, Spika wa bunge hili Philemon Sabulei alitaja mswada wa kutoa mikopo kwa vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu.

Spika huyo anayeondoka aliitaka serikali itakayochukua usukani baada ya uchaguzi mkuu kuhakikisha mswada huo umekuwa sheria akisema utachangia pakubwa kuimarisha uchumi wa vikundi hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuvunjwa kwa bunge hilo, Sabulei pia alitaja mswada wa mazingira utakaohakikisha utunzaji bora wa mazingira katika kaunti hiyo.

Spika huyo alisema licha ya kuvunjwa kwa bunge hilo, wawakilishi wodi wataendelea kutenda kazi yao ya uwakilishi na kusimamia utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo hadi tarehe 9 Agosti wakati wawakilishi wodi wapya watakapochaguliwa.

Alisema bunge hilo lilitenga fedha na wakati kuhakikisha kwamba wananchi wanashirikishwa katika uongozi kama inavyohitajika kisheria.

Sabulei aliwashukuru viongozi mbali mbali katika kaunti hiyo akisema walichangia ufanisi wa kazi za bunge hilo.

admin

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *