Leo ni siku ya mwisho kwa unga wa mia

Wasagaji unga wa kiwanda cha Kajiado Flour Millers wameeleza KNA kuwa kufuatia kutamatisha kwa kandarasi na makubaliano ya kuuza unga kwa bei nafuu, kampuni hiyo ina hadi leo pekee kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya shilingi mia kwa pakiti ya kilo mbili za unga.

“Baada ya leo, tutaweka bei mpya ya unga kwa wateja lakini contract ikirudishwa tutaendelea kuuza kwa bei ya mgao kwa shilingi mia moja kwa kilo mbili za unga wa ugali,” Ali Abdi kutoka Kajiado Millers alisema

Abdi alidokeza kwamba kwa wakati huu wanauza kuanzia bandri kumi na zaidi kwa wauzaji wa rejareja na jumla.

Maelfu ya wakaazi walifurika kwenye duka la Kajiado Millers siku ya jumanne tarehe 17 Agosti 2022 kujipatia unga huo wakisimulia furaha yao kwa kushuka bei ya bidhaa hii muhimu.

Sasa wanaisihi serikali kuzidisha muda wa kandarasi kwa wasaga unga ili waweze kuendelea kupata unga kwa bei nafuu kukithi mahitaji ya chakula kwa jamii zao wakati huu mgumu wa kiangazi.

Hapo juzi, Naidoo Lekeruku, mkaaji wa Kajiado alibahatika kupata kilo ishirini kwa bei ya shilingi elf moja na kupeleka nyumbani kwake kulisha jammaa.

Naidoo alisimulia hali ilivyo kukumbana na hasara ya kupoteza ng’ombe waliofariki tokana na kiangazi akisema kuwa hata maziwa ya ngombe waliotegemea kama njia ya mapato imeadimika hivyo hawana njia mbadala ya kujikimu kimaisha.

“Wakati bei ya unga ilikuwa mia mbili, kwa boma yangu ya watu kumi na tatu hatungeweza kupika ugali yakutosha bali tulipika uji kwa wiki mbili kwani hatukuwa na pesa ya kutosha kununulia unga,” Naidoo alisimulia.

Kufuatia kufanikisha na kupunguza bei ya unga, itabaki mtihani kwa Naibu Rais ambae sasa ni Rais mteule kuboresha maisha ya wakenya kudhibiti mfumko wa bei ya vyakula na petroli.

Wiki moja baada Rais mteule Dkt William Ruto kutangazwa mshindi, wananchi wanasubiri kwa hamu kupunguziwa chakula hiki kulingana na ahadi zake wakati wa kampeni za kura alizoshinda kulingana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Wafula Chebukati.

Lishe bora ni mojawapo ya haki za kibinadam ulimwenguni na kutambuliwa kwenye katiba ya Kenya.

Endapo chakula kinakosekana hasa kwa watoto, mama wajawazito na wazee huthoofika kiafya hadi kupata magonjwa kama utapia mlo kwa watoto na magonjwa mengine kwa watu wazima.

Hali hii ya kukosa chakula na kupata maradhi tofauti huchangia umaskini zaidi kwani pesa nyingi hutumika kugharamia matibabu na kusababisha ukosefu wa hela za matumizi mengine ya kijamii kama elimu na kadhalika.

admin

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *